top of page

TOA SADAKA KWA KADI YA BENKI

Screen Shot 2019-11-15 at 7.42_edited.pn

TOA SADAKA KWA CASHAPP

(Tumia: 202 913 8912)

(Andika: "Sadaka/Zaka/..., au sababu ya malipo)

Ikiwa ungependa kumtolea Mungu sadaka yako kwa njia Kadi ya Benki au Bank Transfer, au Cash App, tafadhali bonyeza sehemu husika hapo juu. Mungu akubariki sana kwa kumrudishia shukrani kwa njia ya matoleo. 

JITOLEE KATIKA HUDUMA

Kama unapenda kujitolea katika moja ya huduma yeyote kanisani kwetu, usisite kuwasiliana nasi.

*For applicable policies on refund and data privacy, please click here >>

KWANINI TUMTOLEE MUNGU?

Ukimtolea Mungu, anakubariki kwa namna ya pekee, sawasawa na neno lake katika Malaki 3:10-12:

"Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu. Mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nanyi kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi."

 

Matoleo yako yanaliwezesha kanisa kuendesha kazi ya Mungu, na kuifikia jamii inayotuzunguka, na kubadilisha maisha ya watu. Sadaka yako inatumika:

  • Kukidhi mahitaji ya gharama za uendeshaji wa huduma za kanisa, kama vile gharama za jengo (rent), vyombo vya mziki na sauti, machapisho mbalimbali, mahitaji ya watoto, usafiri, uendeshaji wa tovuti ya kanisa (website), kukarimu wageni, na matukio mengine ya huduma za kanisa.

 

  • Kuwahudumia chakula, mavazi na mahitaji mengine watu wenye uhitaji, na kuwawezesha kufika kanisani kupata huduma ya kiroho, mafundisho ya ukombozi wa kifikra, pamoja na kuwajengea ushirika wa kijamii. 

Image by Ian Schneider
Clothes Donation
Image by Jon Tyson
Image by Nina Strehl
bottom of page