top of page

HUDUMA ZETU

BECOME A PART OF OUR FAMILY

I'm a paragraph. Click here to add your own text and edit me. It’s easy. Just click “Edit Text” or double click me to add your own content and make changes to the font. I’m a great place for you to tell a story and let your users know a little more about you.

Image by Haley Rivera

Maombi

Huduma hii ni mhimili mkuu wa huduma zote ndani ya kanisa. Ni desturi yetu kukakabidhi kila huduma na shughuli ya kanisa mikononi mwa Mungu kwa njia ya maombi. Waumini wote wanakaribishwa kushiriki. Wasiliana nasi kufahamu ratiba ya maombi. Karibu tuzungumze na Bwana!

Image by Richie Lugo

Uimbaji

Mungu ametubariki na kwaya ya The Sound of Glory ambayo inatuongoza katika kumsifu na kumwabudu Mungu kwa mahadhi ya Kiafrika. Pamoja na kuhudumu katika ibada za kila Jumapili, The Sound of Glory wanafanya matamasha ya kusifu na kuabudu kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, yakiambatana na maombi, na maombezi. 

Evangelist.jpeg

Uinjilisti

Tumeagizwa na Bwana Yesu kuenenda "ulimwenguni mwote kuihubiri injili kwa watu wote, na kila atakayeamini na kubatizwa ataokolewa" (Marko 16:15-16). Tunapeleka injili ndani na nje ya kanisa, na kuwahudumia watu wenye mahitaji ya kiroho na kimwili. Huduma hii ni ya kila mshirika. Uinjilisti ni sehemu ya maisha yetu, kila mahali tunasimama kuwa ishara ya nuru ya Kristo.

AfricanKids.jpeg

Watoto na Vijana

Mtoto aliyelelewa katika maadili ya ya neno la Mungu ni baraka katika jamii na ulimwenguni kote.  Mungu ameweka watu wenye mzigo na wito wa kufundisha watoto na vijana katika kumjua Kristo. Tuna matukio na programu mbalimbali ambazo zinavutia watoto, na kuwaepusha na mambo ya yasiyofaa.

Image by Eric  Froehling

Familia na Ndoa

Familia imara inajenga kanisa imara, jamii imara, na taifa imara. Tunajifunza kumweka Kristo kama msingi wa ndoa na familia zetu.  Huduma hii ina programu mbalimbali za kudumisha mshikamano wa familia ndani ya kanisa. 

Image by Clem Onojeghuo

Wanawake

"Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa;..." (Zaburi 68:11b). Tunakukaribisha mwanamke kujiunga na jeshi letu katika kutangaza habari njema. Karibu tuombe pamoja, tujifunze, na tutiane moyo. Kwa pamoja, tunoane kuwa wanawake mahiri katika ufalme wa Mungu na familia zetu.

Image by Jack Sharp

Wanaume

Wanaume wamebeba jukumu kubwa katika nyumba ya Mungu na familia zao. Mwanaume, karibu tujenge ufalme wa Mungu. Utapata ushirika, na kutiwa moyo na wanaume wengine katika kutimiza kusudi lako hapa duniani.

Image by George Lakos

Usafiri

Huduma ya usafiri inawezesha waumini wapya na wenyeji watokao maeneo yasiyo na usafiri mathubuti, kufika kanisani kwa aijli ya ibada ya Jumapili. Kanisa lina gari mahususi kwa ajili ya huduma hii. 

Welcome_edited_edited.jpg

UKARIMU

Huduma hii inaratibiwa kuhakikisha kila mgeni anayefika kanisani anajisikia yuko kati kati ya ndugu zake katika Kristo. Ikiwa utashiriki ibada nasi kwa mara ya kwanza, tutakuwa tayari kukupokea. Nyote mnakaribishwa!

bottom of page